KSW 1123: Utangulizi wa Fasihi Katika Kiswahili SEP - DEC 2025

Course categoryLMS Training

 

 

KAG EAST UNIVERSITY

UTANGULIZI WA FASIHI KATIKA KISWAHILI

KSW: 1123

MUDA WA KIPINDI: SAA 3

MHADHIRI: EMMAH ACHIENG

NAMBARI YA SIMU: 0790982044

 BARUAPEPE:emmah.achieng@east.ac.ke

 

 

 

 

 

MADHUMUNI YA KOZI

Kozi hii inalenga kumpa mwanafunzi nafasi ya kuielewa fasihi. Kozi itazingatia kwa jumla mambo ya kimsingi yanayohusiana na taaluma ya fasihi. Lengo maalum ni kuhakiki na kuchanganua mbinu mbalimbali za fasihi kwa kuzingatia tanzu mbalimbali za fasihi.

 

Kozi hii itachangia katika kutimiza malengo ya CHUO KIKUU CHA KAG MASHARIKI kwa sababu inahusiana na chuo hiki kama taasisi ya elimu. Kila mwanafunzi anatarajiwa kutimiza malengo ya taasisi hii atakapokuwa akifanya kazi katika sehemu mbalimbali za kazi.

 

CHUO KIKUU CHA KAG MASHARIKI ni taasisi ya Kipentekoste inayodhamiria kuwaandaa viongozi watumishi watakaoleta mabadiliko chanya kote duniani kwa kuishi maisha mema na kufanya huduma inayoongozwa na Roho Mtakatifu.

 

Malengo ya Kozi

Kufikia mwisho wa kozi hii mwanafunzi aweze:

1. Kupambanua dhana ya fasihi kwa jumla

2. Kutathmini umuhimu wa fasihi katika jamii ya kisasa.

3. Kubainisha tofauti zilizoko za umbo na mtindo katika nyanja / tanzu za fasihi

4. Kuhakiki vipengele muhimu katika tanzu za fasihi kama aina za riwaya, tamthilia, ushairi, ploti, vitushi, arudhi, jukwaa, wahusika, tamathali za usemi na kadhalika.

5. Kujadili mwingiliano uliopo kati ya tanzu na vijitanzu vya fasihi ya Kiswahili.

6. Kuchambua kazi za fasihi ya Kiswahili.

7. Kutafiti aina za fasihi zinazopatikana katika jamii yake.

 

MAELEZO

Dhana ya fasihi; maana ya fasihi; chanzo cha fasihi; vipengele vya fasihi; fasihi simulizi: maana yake, tanzu na vipera vyake; fasihi andishi: riwaya, maana ya riwaya, historia ya riwaya, aina za riwaya, fani na maudhui katika riwaya/dhamira, uchambuzi wa riwaya; hadithi fupi: maana ya hadithi fupi, fani na maudhui; tamthilia: maana ya tamthilia, historia ya tamthilia, uhakiki wa tamthilia; ushairi: maana ya ushairi, historia ya ushairi, aina za ushairi, uchambuzi wa ushairi.

 

Kama taasisi ya Kikristo ya elimu ya ngazi za juu CHUO KIKUU CHA KAG MASHARIKI inashughulika mno na kujenga mtazamo wa Kikristo kuhusu elimu. Katika chuo kikuu hiki, Ukristo uliomo katika biblia ndio msingi wa mpango mzima wa elimu au mkondo ambao mto wa kufunza na kusoma unatiririkia. Kwa hivyo, ni jukumu la mhadhiri kuwapa wanafunzi mitazamo ya biblia katika kila somo na zoezi. Kwa maneno mengine, kuambatisha biblia na elimu kunahitajika.

 

 

 

 

JUMA

MADA

MADA NDOGO

MALENGO

UMILISI

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

SHUGHULI ZA MHADHIRI

SHUGHULI ZA WANAFUNZI

1

Dhana ya fasihi

Fasili mbalimbali za Fasihi

 

Chanzo cha fasihi

LENGO 1

Uwezo wa mawasiliano na ushirikiano(wanafunzi wanapojadiliana na wenzao na kutoa fasili mbalimbali za fasihi)

Ujuzi wa kidijitali(ywanapotafuta fasili mbalimbali za fasihi mtandaoni

Kuuliza maswali kuhusu fasili mbalimbali za fasihi

 

Kuwaeleza wanafunzi kuhusu chanzo cha fasihi

Kuandika

 

Kujadiliana na Kutoa fasili zao kuhusu fasihi

 

 

2

Vipengele vya fasihi; Fasihi simulizi: maana yake, tanzu na vipera vyake;

 

Maana ya fasihi simulizi

 

Tanzu na vipera vya fasihi simulizi

LENGO 4

Mawasiliano na ushirikiano(wanapojadiliana kuhusu tanzu na vipera vya fasihi  

Kuwaeleza wanafunzi kuhusu tanzu na vipera vya fasihi simulizi

Wanafunzi kujadilina kufafanua tanzu na vipera vya fasihi simulizi

3

Fasihi andishi:Riwaya 

 

Maana ya riwaya, Historia ya riwaya

Aina za riwaya

LENGO

4

Ufanisi wa kibinafsi(wanapoeleza maana ya riwaya na historia yake na aina za riwaya

Kueleza maana ya riwaya na historia yake

Wanafunzi kueleza maana ya riwaya

Wanafunzi kutafiti mtandaoni kuhusu historia ya riwaya na aina za riwaya

4

MUJARABU WA KWANZA(KAZI YA KIBINAFSI-10%

 

 

Kufikiri  kwa makini na kutatua matatizo, mawazo (mwanafunzi anapojibu maswali)

 

 

5

Fasihi andishi:Riwaya

 

Fani na maudhui katika riwaya/dhamira, uchambuzi wa riwaya

 

LENGO 4,6

Ujuzi wa kidijitali (kutafuta mtandaoni fani na maudhui katika riwaya )

Kueleza fani na maudhui katika riwaya

Wanafunzi kujadili vipengele vya kuzingatiwa katika uchambuzi wa riwaya

 

Kuandika

6

Hadithi fupi

Maana ya hadithi fupi, fani na maudhui

 

LENGO 4,6

Mawasiliano na ushirikiano(wanapoeleza maana ya hadithi fupi na kuichambua)

Kuuliza maswali

 

Wanafunzi kusoma na kuchambua hadithi fupi 

7

Tamthilia

Maana ya tamthilia, historia ya tamthilia, uhakiki wa tamthilia

LENGO 4,6

Mawasiliano na ushirikiano(wanapoeleza maana na historia ya tamthilia)

 

Ubunifu(wanapochambua tamthilia)

Kuwaelekeza wanafunzi katika kueleza historia ya tamthilia na uhakiki wake)

Wanafunzi kueleza maana ya tamthilia na historia yake 

 

Wanafunzi kuhakiki tamthilia

8

MUJARABU WA PILI (MAKUNDI NA UWASILISHAJI)- 10%

 

 

 

Mawasiliano na ushirikiano, ujuzi wa kidijitali,ubunifu, kufikiri na kutatua matatizo

 

 

9

Ushairi

 

Maana ya ushairi, Historia ya ushairi, Aina za ushairi, Uchambuzi wa ushairi.

 

LENGO 4,6

Mawasiliano na ushirikiano(wanapojadiliana na kuwasilisha kuhusu ushairi)

Kueleza maana ya ushairi, historia na aina za ushairi

 

Wanafunzi kujadiliana kuhusu historia na aina za ushairi

 

Wanafunzi kuchambua mashairi mbalimbali 

10

Ushairi

Uchambuzi wa ushairi.

LENGO 4,6

Mawasiliano na ushirikiano(wanapochambua mashairi mbalimbali)

Kuchambua mashairi mbalimbali

Wanafunzi kusoma na kuchambua mashairi mbalimbali

Kuandika

11

MAREJELEO YA KOZI

 

 

 

 

 

12

 

MAREJELEO YA KOZI

 

 

 

 

 

13-14

 

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA- 40%

 

 

 

 

 

 

 

MBINU ZA KUFUNZIA

Mihadhara darasani, Majadiliano kuhusu mada mbalimbali darasani, Mawasilisho kuhusu mazoezi mbalimbali, utafiti wa maktabani na mtandaoni.

 

VIFAA VYA KUFUNZIA

Ubao wa kuandikia, mtandao, vitabu vya Fasihi, nakala za kusoma.

 

UTAHINI

Mahudhurio na Kushiriki: 10%

Mjarabu wa kwanza (wa kibinafsi) 10%

Mjarabu wa pili (Makundi na Uwasilishaji) 10%

Mjarabu wa tatu (Karatasi ya Muhula) 20%

Mjarabu wa nne (kazi ya makundi ya pili) 10%

Mtihani wa mwisho 40%

JUMLA 100%   

MAKATAA

Mjarabu wa kwanza- wiki ya 4

Mjarabu wa pili(makundi na uwasilishaji)- wiki ya 8

Mjarabu wa tatu(karatasi ya muhula)- Wiki ya 9

Mjarabu wa nne (kazi ya makundi ya pili)-wiki ya 9

Mtihani wa mwisho- wiki 13-14

 

 

MAREJELEO

Abedi, K. M. (1965). Sheria za kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: Kenya Literature Bureau.  

 

Njogu, K. & Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.

 

Wamitila, K.W. (2003). Kichocheo cha Fasihi: Simulizi na Andishi. Nairobi: Focus Books.

Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books.

 

Wamitila, K.W. (2008). Kanzi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi: Vide-Muwa Publishers.

 

 

 

 

 

 

 

 

Lecturer: Emmah Achieng